Msuva akimbiza ligi kuu ya Morocco

Winga wa zamani wa Yanga Simon Msuva ambaye sasa anachezea klabu ya Difaa El Jadida inayoshiriki ligi kuu nchini Morocco, nyota yake imezidi kun'gara.

Msuva amekuwa mchezaji pekee kutoka klabu ya Difaa kuingia kwenye orodha ya kikosi bora cha ligi kuu ya Morocco kwa mwezi Novemba.

Tayari Msuva ameifungia Difaa El Jadida mabao matano kwenye ligi kuu nchini humo.

Inadaiwa kuwa klabu ya Malaga inayoshiriki ligi kuu ya Hispania, La Liga imevutiwa nae huenda akasajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili mwezi ujao kama atafuzu majaribio.