Ratiba ya kombe la Azam FA hadharani

Ratiba ya hatua ya awali kombe la FA imetangazwa na shirikisho la soka nchini (TFF) kwa kushirikiana na wadhamini wa michuano hiyo kampuni ya Azam.

Michezo ya mzunguuko wa pili inayohusisha timu 64 kutoka timu za ligi daraja la pili, la kwanza na ligi kuu inatarajiwa kupigwa kati ya Disemba 20 na 25.

Yanga, Azam FC na Simba zimepangwa na timu za daraja la pili na la kwanza.

Yanga itachuana na Reha FC, Simba itachuana na Green Worriers wakati Azam FC itapambana na Area C FC.

Ratiba kamili
JKT Mlale vs KMC
Ambassador vs JKT Oljoro
Mshikamano vs Polisi Tanzania
Rhino Rangers vs Alliance
Ashanti United vs Friends Rangers
Toto Africans vs Eleven Stars
Majimaji Rangers vs Mbeya Kwanza
Mirambo FC vs Buseresere

African Lyon vs Kiluvya United
Biashara Mara vs Mawenzi Market
Mvuvumwa vs JKT Ruvu
Coastal Union vs Dodoma FC
Polisi Dar vs Mgambo JKT
Kariakoo Lindi va Transit Camp
Shupavu FC vs Real Mojamoja
Mufindi United vs Pamba FC

Kagera Sugar vs Makambako Heroes
Ruvu Shooting vs Madini FC
Abajalo vs Prisons
Njombe Mji vs Mji Mkuu
Singida United Vs Bodaboda
Mwadui vs Pepsi FC
Majimaji FC vs New Generation
Boma FC vs Ndanda
Stand United vs AFC

Burkinafaso vs Lipuli
Green Worriers vs Simba
Azam vs Area C
Yanga vs Reha
Mbeya City vs Ihefu FC
Villa Squad vs Mtibwa Sugar
Makanyagio vs Mbao FC