Kikosi cha Taifa Stars kilichoshiriki AFCON 1980

Aliyewahi kuwa Mkuu wa mikoa ya Morogoro na Manyara kwa nyakati tofauti Joel Nkaya Bendera amefariki jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikofikishwa kupatiwa matibabu mapema hiyo jana.

Bendera aliwahi kuwa Waziri kwenye Serikali ya awamu iliyopita, pia licha ya kujihusisha na siasa, Bendera alikuwa ni kocha aliyesomea.

Alipata kufundisha timu ya Taifa ya Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 1980.

Bendera ndiye aliyeongoza kikosi cha timu ya Taifa kushiriki fainali ya michuano ya mataifa barani Afrika kwa mara ya kwanza nchini Nigeria mwaka 1980.

Tanzania haijawahi tena kupata nafasi hiyo hivyo kumfanya Bendera aondoke duniani huku akiwaachia mtihani walimu wa Taifa Stars kuifikia rekodi yake.

Pichani juu ni kikosi cha 'Kilimanjaro Stars', kilichoshiriki katika michuano ya kombe la Chalenji ya 1984.

Kushoto kwa Mzee Kawawa, ni Kocha Wolk, na nayefuatia ni Kocha Msaidizi Joel Bendera.