Simba yaipania Singida United

Kikosi cha Simba kimeanza mazoezi jana kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Singida United Alhamisi ijayo.

Baada ya kutoka visiwani Zanzibar ilikokwenda kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi, wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja.

Simba imebakiza Ligi Kuu Bara pekee ambako watapambana kupata ubingwa baada ya kuwa wamevuliwa ubingwa wa Kombe la Shirikisho.

Ni lazima Simba itwae ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom ili iweze kushiriki michuano ya Kimataifa mwakani.

Simba inajifua kwenye Uwanja wa Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam.