Guardiola kocha bora wa mwezi Disemba

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola ametwaa tuzo ya Meneja bora wa mwezi kwa mara ya nne mfululizo.

Guardiola ameweka rekodi mpya ya kutwaa tuzo hiyo katika ligi kuu ya Uingereza.

Mwenendo wa kutofungwa wa Manchester City unamuwezesha meneja huyo kutoka Catalunya kutwaa tuzo hiyo.

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Disemba, 2017.