Ligi ya Mabingwa Ulaya kuendelea leo

Ligi ya Mabingwa hatua ya mtoano imerejea! Michezo ya mzunguuko wa kwanza hatua ya 16 bora inatarajiwa kuanza kupigwa leo.

Leo kutakuwa na michezo miwili ambapo Juventus itakuwa na mtihani mgumu itakapoikaribisha Tottenham Hotspurs iliyo katika iwngo bora.

Fc Basel itakumbana na vinara wa ligi kuu ya Premia, Manchester City.

Michezo yote inatarajiwa kuanza saa tano kasorobo usiku.

Kesho Jumatano kutakuwa na michezo miwili pia ambapo FC Porto itaikaribisha Liverpool FC huku Real Madrid ikikumbana na kikosi bora barani Ulaya kwa sasa, PSG.

Michezo mingine inatarajiwa kupigwa wiki ijayo.