Yanga kuifuata St Louis Jumapili

Wakati mikakati ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Majimaji Fc kwenye mfululizo wa ligi kuu ya vodacom jumatano hii,kikosi cha Yanga kinatarajia kuondoka jumapili asubuhi kuelekea Shelisheli tayari kwa mchezo wa marejeano na mabingwa wa nchi hiyo St Louis.

Katibu Mkuu wa Yanga Sc, Charles Mkwasa,amesema matayarisho ya safari hiyo tayari yamekwisha kamilika ikiwa ni pamoja na taratibu za usafiri kwa wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi.

"Matayarisho yameshafanyika, jumla ya wachezaji 20 na viongozi 10 wakiwemo wanane wa benchi la ufundi,tunafahamu mchezo utakuwa tarahe 21/2 hivyo tumeona umuhimu wa kwenda mapema ili kupata wasaa wa kuzoea mazingira na kucheza tukiwa hatuna presha ya hali ya hewa."

Kuhusu Mchezo wa Majimaji Mkwasa alisema,kikosi kinatarajia kuingia kambini kesho kwenye hotel ya Zimbo tayari kwa mchezo huo wa kesho kutwa uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

"Maandalizi yamekamilika,timu inaingia kambini kesho,mchezo huu ni muhimu kwetu na tumeupa uzito kutosha kwa sababu tunahitaj kushinda,Majimaji ni timu nzuri tunajua utakuwa mchezo wenye upinzani wa hali ya juu."