Simba yaifuata Mwadui FC leo

Baada ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha Simba kinakwenda mkoani Shinyanga tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 18.

Alhamisi February 15 Simba, vinara wa ligi Kuu, watakuwa ugenini mkoani humo kuivaa Mwadui FC.

Kocha Msaidizi wa Simba Masudi Djuma amesema wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya Mwadui FC ili kuhakikisha wanabaki kileleni kwa tofauti ya alama nyingi dhidi ya wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa.

Aidha matokeo ya sare iliyopata Azam FC jana, yanazidi kuiweka Simba katika nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa.

Kwani kama itapata ushindi dhidi ya Mwadui FC itaizidi timu hiyo kwa alama 10.