Messi hazuiliki - Morata

Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata amewata wachezaji wa timu hiyo kucheza kwa tahadhari kubwa kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa wiki ijayo dhidi ya FC Barcelona.

Jumanne ijayo Februari 20, Chelsea itaikaribisha Barcelona kwenye dimba la Stamford Bridge kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano, ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Morata ametahadharisha kuwa Chelsea itakumbana na timu yenye mchezaji ambaye si rahisi kumzuia, Messi.

Morata amesema ili kuweza kufuzu ni lazima wapate ushindi kwenye mchezo wa kwanza lakini itawalazimu wawe makini zaidi kama timu kufanikiwa kuepeka 'balaa' la Messi.

Chelsea ina kumbukumbu ya kuiondosha FC Barcelona kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mwaka 2012 kwa kuichapa jumla ya mabao 3-2.

Lakini safari itabidi wajipange kweli kwani watakutana na timu ambayo inaongoza ligi kuu ya Hispania, La Liga huku ikiwa imecheza michezo 23 ya ligi bila kufungwa.