Yanga yaenda Botswana

Baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Stand United jana, kikosi cha Yanga kimeondoka usiku wa kuamkia leo kuelekea nchini Botswana tayari kwa mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers.

Yanga itaikabili Township Rollers Jumamosi ijayo, March 17 katika mchezo ambao inahitaji ushindi ili kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Matokeo ya kipigo cha 2-1 ya mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam wiki iliyopita, yanaifanya Yanga ilazimike kushinda ugenini kwa angalau mabao 2-0