Tshishimbi mchezaji bora wa VPL February

Kiungo wa Yanga Papi Kabamba Tshishimbi amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi wa pili Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Katika mwezi wa pili Tshishimbi aliisaidia Yanga kushinda michezo yake yote minne ya ligi huku pia akifanikiwa kufunga mabao matatu.

Katika mwezi huo Tshishimbi alifunga moja ya mabao wakati Yanga ilipoichapa Lipuli FC mabao 2-0 na akawemo kwenye kikosi cha Yanga kilichoichapa Njombe Mji mabao 4-0.

Pia alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 4-1 iliyopata Yanga dhidi ya Majimaji, akawemo kwenye kikosi cha Yanga kilichoichapa Ndanda FC mabao 2-1.

Tshishimbi ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda Pius Buswita wa Yanga na Emanuel Okwi wa Simba

Tshishimbi amekuwa katika kiwango bora tangu ajiunge na Yanga mwanzoni mwa msimu akitokea Mbabane Swallows.