Kane aipa hofu Uingereza

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Harry Kane aliumia kifundo cha mguu juzi wakati timu yake ikiichapa Bournemouth mabao 4-1 katika mchezo wa Premia Ligi.

Kane alitoka nje kwenye dakika ya 30 baada ya kugongana na mlinda lango wa Bournemouth, Asmir Begovic.

Kane anatarajiwa kuwa nje kwa wiki kadhaa. Kuumia kwake kunaipa hofu Spurs inayosaka moja ya nafasi nne za juu lakini hofu zaidi kwa Uingereza inayomuhitaji sana katika michuano ya kombe la dunia miezi mitatu ijayo.

Kane amefunga mabao 24 kwenye ligi kuu ya Uingereza msimu huu akiwa amefungana na Mohammed Salah wa Liverpool.

Amefunga mabao 35 kwenye michuano yote