Simba vs Prisons uwanja wa Taifa leo

Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Simba leo wanashuka kwenye uwanja wa Taifa kuwakabili maafande wa Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 24.

Simba inayoongoza ligi ikiwa imejikusanyia alama 55, inahitaji kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo ili kuukaribia zaidi ubingwa wa msimu huu.

Matokeo ya ushindi yataifanya Simba ipae kileleni kwa taofauti ya alama 11 dhidi ya mahasimu wao Yanga ambao wana alama 47 wakiwa wamecheza michezo 22.

Yanga iko nchini Ethiopia kucheza mchezo wa marudiano kombe la shirikisho dhidi ya Wolaitta Dicha.

Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema licha ya hali ya hewa kutokuwa rafiki, maandalizi ya kuelekea mchezo huo yamekamilika.

Naye Kocha Msaidizi wa Simba Masudi Djuma amesema michezo yote iliyobaki ni fainali kwao hivyo wamejipanga kuhakikisha wanashinda.