Msimamo baada ya mzunguuko wa 25 kukamilika

Ushindi wa mabao 2-0 iliyopata Simba dhidi ya Prisons leo unaifanya iongoze ligi kwa tofauti ya alama 11 dhidi ya Yanga iliyo nafasi ya pili.

Yanga ina michezo miwili ya kiporo.

Kagera Sugar baada ya kuilaza Mtibwa Sugar kwa mabao 2-1 imeondoka kwenye eneo la kushuka daraja kwa kupanda hadi nafasi ya 12 baada ya kufikisha alama 26.

Ruvu Shooting huenda ikawa imejihakikishia kubaki ligi kuu msimu ujao baada ya kuilaza Ndanda FC mabao 3-1 hivyo kujikita nafasi ya saba ikifikisha alama 32.

Hali bado ni tete kwa Njombe Mji, Majimaji, Ndanda na Mbao FC ambazo licha ya kuwa kwenye eneo la hatari, zimefungwa au kuambulia sare kwenye michezo yao ya mzunguuko wa 25